Hali Ngumu ya Waandishi wa Habari Kenya: 52% Wanalipwa Chini ya KSh 50,000, Utafiti Wafichua Changamoto Kazini.

Our Community

JamiiCheck(https://www.jamiiforums.ke/forums/139/)

FichuaUovu(https://www.jamiiforums.ke/forums/137/)

Stories of Change(https://www.jamiiforums.ke/categories/stories-of-change)

Start Discussion(https://www.jamiiforums.ke/forums/-/create-thread)

Coming Soon

JamiiCourses(https://www.jamiiforums.ke/lessons)

JamiiData(https://www.jamiiforums.ke/categories/jamiidata-infographic-portal.172)

JamiiShop(https://www.jamiiforums.ke/jamiishop)

Premium Content(https://www.jamiiforums.ke/forums/)

Regional Communities

Coming Soon

Tanzania

Uganda

Kenya

Rwanda

DRC

Zambia

Zimbabwe

Menu

Log in(https://www.jamiiforums.ke/login/)

Register(https://www.jamiiforums.ke/register/)

Navigation

More options

Style variation(https://www.jamiiforums.ke/misc/style-variation)

System(https://www.jamiiforums.ke/misc/style-variation?reset=1)

Light(https://www.jamiiforums.ke/misc/style-variation?variation=default)

Dark(https://www.jamiiforums.ke/misc/style-variation?variation=alternate)

Contact us(https://www.jamiiforums.ke/misc/contact)

Close Menu

You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly. You should upgrade or use an alternative browser(https://www.google.com/chrome/).

Forums(https://www.jamiiforums.ke/forums/)

Africa Regional Specific Forums(https://www.jamiiforums.ke/forums/#africa-regional-specific-forums.116)

Kenyan News and Politics(https://www.jamiiforums.ke/forums/kenyan-politics.115/)

Hali Ngumu ya Waandishi wa Habari Kenya: 52% Wanalipwa Chini ya KSh 50,000, Utafiti Wafichua Changamoto Kazini.

Thread starter

Ikariiah(https://www.jamiiforums.ke/members/ikariiah.559679/)

Start date

Today at 9:18 AM(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/)

I(https://www.jamiiforums.ke/members/ikariiah.559679/)

Ikariiah(https://www.jamiiforums.ke/members/ikariiah.559679/)

JF-Expert Member

Jul 17, 2019

275

306

Today at 9:18 AM(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/#post-57150004)

#1(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/#post-57150004)

Zaidi ya nusu ya wanahabari nchini Kenya wanapata mshahara wa chini ya shilingi 50,000 kwa mwezi, huku wengi wakikabiliwa na changamoto za ajira zisizo za kudumu, kutopandishwa mishahara na kukosa marupurupu ya kikazi.

Hayo ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa State of Journalists’ Welfare Survey, uliofanywa na Chama cha Wanahabari Kenya (KUJ) kwa ushirikiano na Baraza la Habari Kenya (MCK), ukiwahusisha wanahabari 120 kutoka vyombo mbalimbali vya habari na ngazi tofauti za taaluma.

Utafiti huo uliozinduliwa Oktoba 30, 2026, umebaini kuwa 52% ya waliohojiwa wanapata chini ya 50,000 kwa mwezi, huku wastani wa mshahara wa wanahabari hao ukiwa 63,000.

Aidha, 55% ya washiriki wanafanya kazi kama waandishi wa maeneo (correspondents), wanahabari wa kujitegemea (freelancers) au wachangiaji wa maudhui (contributors), badala ya kuwa na ajira za kudumu.

Hali ya mishahara nayo imeibua wasiwasi, huku 48% ya wanahabari wakisema hawajapitiwa upya mishahara yao kwa zaidi ya miaka mitatu. Wakati huohuo, 82% walisema hawapati marupurupu ya ziada wala bonasi kutoka kwa waajiri wao.

Wanahabari wengi wanatafuta ajira kwingine .

Utafiti huo umebaini kuwa 89% ya correspondents waliohojiwa wanatafuta ajira nje ya maeneo yao ya sasa ya kazi, huku mmoja kati ya wanahabari watatu akisema ana mpango wa kuondoka katika taaluma ya uandishi wa habari akipata fursa tu.

Hata hivyo, si wote wanaotaka kuondoka kwenye tasnia ya habari; baadhi wanatafuta nafasi bora katika vyombo vingine vya habari, huku wengine wakitafuta fursa nje ya taaluma hiyo.

Kwa upande wa mazingira ya kazi, wanahabari wanasemekana kufanya kazi wastani wa saa 8.5 kwa siku, huku zaidi ya 65% wakiripoti kuongezeka kwa mzigo wa kazi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita bila ongezeko linalolingana la mishahara au marupurupu.

Afya ya akili ya waandishi pia imeibua wasiwasi .

Utafiti huo pia umeangazia hali ya ustawi wa kihisia miongoni mwa wanahabari. Kwa kutumia kipimo cha PHQ-9, 65% ya washiriki walionyesha dalili za wastani hadi kali za msongo unaohusiana na hali ya sonona.

Ni 25% pekee waliokuwa wametafuta msaada wa kitaalamu wa afya ya akili katika kipindi cha miaka 2 iliyotangulia utafiti huo. Ni muhimu kufahamu kuwa PHQ-9 ni kipimo cha kuchunguza dalili, si utambuzi wa kitabibu kwamba mtu ana sonona.

Akizungumzia matokeo hayo, Katibu Mkuu wa KUJ, Eric Oduor, amesema haiwezekani kutarajia mwandishi ambaye hapati malipo yanayostahili kutekeleza kikamilifu jukumu la kuiwajibisha Serikali, kusema ukweli na kutetea maslahi ya umma.

Kwa upande mwingine, Mamlaka ya Udhibiti wa Mafao ya Kustaafu (RBA) imeahidi kushirikiana na KUJ katika kuanzisha mpango wa pensheni utakaolenga waandishi wanaofanya kazi bila ajira za kudumu, wakiwemo freelancers, correspondents na contributors.

Matokeo haya yanaibua mjadala mpana kuhusu mazingira ya kazi katika tasnia ya habari, hasa wakati wanahabari wanatarajiwa kufanya kazi chini ya shinikizo la muda, kufuatilia masuala ya umma na kuwawajibisha wenye mamlaka.

Wewe una maoni gani kuhusu hali ya maslahi ya wanahabari nchini Kenya? Je, vyombo vya habari vinawalipa na kuwapa mazingira yanayostahili kwa kazi wanayofanya, au tasnia hii inahitaji mageuzi makubwa katika masuala ya mishahara, ajira na ustawi wa wafanyakazi?

Attachments

3597.jpeg

35.1 KB

· Views: 1

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI(https://www.jamiiforums.ke/members/tajiri-mkuu-wa-matajiri.32753/)

JF-Expert Member

Dec 1, 2010

11,935

24,218

Today at 9:19 AM(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/#post-57150013)

#2(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/#post-57150013)

Ikariiah said:(https://www.jamiiforums.ke/threads/hali-ngumu-ya-waandishi-wa-habari-kenya-52-wanalipwa-chini-ya-ksh-50-000-utafiti-wafichua-changamoto-kazini.2489355/#post-57150004)